Skip to main content
RAIS MSTAAFU MHE. KIKWETE AONGOZA KONGAMANO LA MIAKA 40 YA SADC
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiwasilisha salamu za Wizara kwa washiriki (hawapo pichani) katika kongamano la maadhimisho ya miaka 40 ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula. Kongamano hilo limefanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete akiwasilisha mada kuu kwa washiriki wa Kongamano la Maadhimisho ya miaka 40 ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC): Uzoefu wa Tanzania