Waziri wa Mambo ya Nje azungumza na Watumishi wa Wizara
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mahsariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe mara baada ya kuwasili kwenye eneo la Ukumbi wa Mikutano la Informatics lililopo Chuo Kikuu cha Dodoma kwa ajili ya kukutana kwa mara ya kwanza na Watumishi wa Wizara tarehe 23 Machi 2019
Mhe. Prof. Kabudi akizungumza na Watumishi wa Wizara (hawapo pichani) alipokutana nao kwa mara ya kwanza baada ya kuteuliwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye nafasi hiyo tarehe 3 Machi 2019. Pamoja na
Mkutano ukiendelea huku Watumishi wa Wizara wakifuatilia
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Mhe. Prof. Kabudi ambaye haonekani pichani alipozungumza nao
Mhe. Prof. Kabudi alitumia fursa ya mkutano wake na Watumishi wa Wizara kugawa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015 kwa Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara na kuwaagiza kuitekeleza kwani ni miongoni mwa miongozo muhimu katika utekelezaji wa majukumu
Mhe. Waziri (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa meza kuu. Kulia kwake ni Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe na kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizzi wa Ras