WAZIRI MULAMULA AKUTANA NA BALOZI WA MAREKANI NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amefanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Donald Wright leo tarehe 2 Februari 2022 jijini Dodoma. Pamoja na mambo mengine viongozi hao wamejadili juu ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani katika sekta za afya, uwekezaji, biashara na uhusiano wa kimataifa.
  • Kushoto ni afisa kutoka Ubalozi wa Marekani, Bi. Kristin Mencer akifuatilia mazungumzo.
  • Picha ya Pamoja.