Skip to main content
News and Events

Tanzania yakutana na Sekretarieti ya SADC

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa  Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo ameongoza kikao cha Timu ya Tanzania na Sektretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam. 


Lengo la kikao hicho ni kuzipitisha Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali katika majukumu yake wakati wa Uenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ( SADC-Organ) kwa kipindi cha kuanzia Agosti 2024 hadi Agosti 2025.


Itakumbukwa kuwa Mkutano wa 44 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC uliofanyika tarehe 17 Agosti, 2024 ulimchagua Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mwenyekiti wa SADC-Organ kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi Agosti 2025.


Ujumbe wa Sekretarieti umeongozwa na Mkurugenzi wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Prof. Ishmael Theletsane na unatarajiwa kuzitembelea sekta mbalimbali ikiwemo Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili kuziandaa kwa ajili ya kuratibu na kuongoza  Mikutano na Vikao mbalimbali vitakavyofanyika nchini.


Hii ni mara ya nne kwa Tanzania kushika nafasi ya uenyekiti wa Organ. Mara ya kwanza ilikua ni mwaka, 2006/2007; mara ya pili ni 2012/2013 na mara ya mwisho ni  2016/2017.