Skip to main content
News and Events

TANZANIA YAFUNGUA KONSELI KUU GUANGZHOU, CHINA

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 20 Mei 2022 imefungua Konseli Kuu mjini Guangzhou China. Uwepo wa Konseli Kuu katika mji huo kuta iwezesha Tanzania kutumia vyema fursa za biashara na uchumi na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa Watanzania wanaoishi na kufanya shughuli mbalimbali katika mji huo. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akihutubia kwenye hafla ya ufunguzi wa Konseli Kuu hiyo kwa njia ya mtandao alisema kufungua ubalozi huo sambamba na kuendeleza uhusiano mzuri wa kidiplomasia na biashara katika ya Tanzania na China , Konseli Kuu hiyo ni muhimu katika kuhudumia Jumuiya ya Watanzania ambapo ndio idadi kubwa zaidi kuliko miji yote ya China.

"Guangzhou imekuwa mshirika mkubwa wa kibiashara kati ya China na Tanzania ambapo kwa mwaka 2020/2021 kupitia mji huu biashara kati ya Tanzania na China ilifukia shilingi dola za Marekani 6.74. Hivyo ni matumaini yetu kwa kuwa na Konseli Kuu hapa biashara kati ya Tanzania na China itakuwa maradufu” alisema Mhe. Balozi Liberata Mulamula

Konseli Mkuu wa Konseli Kuu ya Tanzania mjini Guangzhou Bw. Khatibu Makenga, akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi alisema Konseli hiyo italeta msukumo mpya wa biashara, uwekezaji na mahusiano ya kiutamaduni baina ya Tanzania na China.

Kwa upande wake Bw. Luo Jun, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya jimbo la Guangdong, akizungumza katika halfa ya ufunguzi alisema mji wa Guanzhou licha ya kuwa ni lango kubwa la biashara kati ya China na Mataifa mengine duniani una historia ya kipekee kwenye historia ya ushirikiano baina ya Tanzania na China. Aliongeza kusema Guangzhou ni kielelezo cha ushirikiano na urafiki wa Tanzania na China.

  • Hafla ya ufunguzi ikiendelea