Skip to main content
News and Events

SALAMU ZA RAMBIRAMBI

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea kwa mshtuko, taarifa za kifo cha Mhe. Bernard Kamillius Membe, aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (2007-2015). Kama Waziri wa Mambo ya Nje aliyehudumu Kwa kipindi Kirefu, atakumbukwa kwa mchango wake katika kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia ya Tanzania na Jumuiya ya Kimataifa. Wizara inatoa pole za dhati kwa familia na watanzania kwa ujumla kwa kumpoteza Mwanadiplomasia mahiri. "Tunaiombea Roho yake ipumzike Kwa Amani"