RAIS WA UJERUMANI FRANK-WALTER STEINMEIER ATAMBELEA KIWANDA CHA TWIGA CEMENT CHA JIJINI DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier ametembelea kiwanda cha kuzalisha saruji cha Twiga (Twiga Cement) kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam.
Rais Frank-Walter Steinmeier amepata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji saruji zinazoendelea kiwandani hapo.
Kiwanda hicho cha Twiga Cement kinachotarajia kuongeza uwekezaji wake kufikia Dola za Marekani Milioni 500 kilijengwa nchini mwaka 1967.
Kiwanda cha Twiga Cement kina ubia na Kampuni ya Scancem International ya nchini Ujerumani.
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akizindua jengo la Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Twiga (Twiga Cement) kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akiangalia moja ya malighafi zinazotumika katika uzalishaji wa saruji alipotembelea Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Twiga (Twiga Cement) kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam
Taswira ya Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Twiga (Twiga Cement) kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akiangalia shughuli mbalimbali za uzalishaji alipotembelea Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Twiga (Twiga Cement) kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam
ais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akiangalia taswira ya Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Twiga (Twiga Cement) kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akiangalia ramani ya Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Twiga (Twiga Cement) jijini Dar es Salaam