RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA TDB

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse wakifurahia jambo mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu jijini Dodoma

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA TDB 

  • Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (katikati), Mkuu wa Itifaki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge (mweji vazi la Jeshi) na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (Watatu kushoto) wakijongea usawa wa ndege kumlaki Rais wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse alipowasili jijini Dodoma Novemba 25, 2019.
  • Picha ya pamoja
  • Rais wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango.