Prof. Kabudi azungumza na Idara ya Itifaki ya Wizara yake.
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akizungumza na Watumishi wa Idara ya Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani) alipokutana nao kwa mara ya kwanza baada ya kuteuliwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye nafasi hiyo tarehe 3 Machi 2019. Pamoja na mambo mengine, Mhe. Prof. Kabudi aliwataka Watumishi wa Wizara kubadilika na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu miongozo na maelekezo mbalimbali pamoja na kuwa wazalendo na kufanya kazi zao kwa kushirikiana na kwa weledi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Mkurugenzi wa Idara ya Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje Mhe. Balozi Grace Martin na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Katika Wizara ya Mambo ya Nje. Aidha, mazungumzo hayo ni mwendelezo wa Vikao vya Prof. Palamagamba John Kabudi na Watumishi wa Wizara yake, ambapo yamefanyika katika Ofisi ndogo jijini Dar es Salaam tarehe 04 Juni, 2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akutana kwa mara ya kwanza na kiting cha Itifaki cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mkurugenzi wa Idara ya Itifaki ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Grace Martini akitoa maelezo ya majukumu ya kitengo hicho kwa Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi alipok