Prof. Kabudi afungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Baraza hilo uliofanyika jijini Dodoma, tarehe 24 Machi 2019. Prof. Kabudi aliwataka wajumbe wa Baraza hilo ambao ni wawakilishi wa watumishi wote wa Wizara kuhakikisha wanatekeleza majukumu kwa kuzingatia vipaumbele vya Wizara ikiwemo Diplomasia ya Uchumi ili kukuza uwekezaji na biashara pamoja na kuvutia utalii kwa maslahi mapana ya Taifa
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Mhe. Prof. Kabudi (hayupo pichani)
Sehemu nyingine ya wajumbe wa Baraza wakati wa mkutano wao wa mwaka
Wajumbe wa Baraza
Mhe. Prof. Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa meza kuu mara baada ya kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushi