Skip to main content
News and Events

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE, MHE. OLE NASHA ALIVYOPOKELEWA WIZARANI

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Ole Nasha ameahidi ushirikiano kwa Watumishi wa Wizara katika kuhakikisha Wizara inakuwa na matokeo chanya yenye tija kwa jamii na Taifa kwa ujumla katika utekelezaji wa majukumu yake.

Mhe. Ole Nasha ameyasema hayo aliwapowasili Wizarani mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika hafla iliyofanyika Ikulu, Chamwino jijini Dodoma tarehe 9 Desemba 2020.

Mhe. Ole Nasha ambaye alipokelewa na Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amesema kuwa yupo tayari kujifunza kutoka kwa Watumishi wote ili kuiwezesha Wizara kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake. Prof. Kabudi alimhakikishia Mhe. Ole Nasha ushirikiano wake binafsi na kutoka kwa Watumishi wote na kwamba uwepo wake utaongeza nguvu za kuifikisha Wizara katika viwango vya juu kiutendaji.

  • Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Ole Nasha akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa Watumishi wa Wizara Bi. Amina Abdallah ikiwa ni ishara ya kukaribishwa mara alipowasili Wizarani baada ya kuapishwa Ikulu tarehe 9 Desemba 2020.
  • Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akimkabidhi Mhe. Ole Nasha Ilani ya Chama cha Mapinduzi kama moja ya kitendea kazi chake anapoanza majukumu yake mapya Wizarani
  • Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Emmanuel Buhohela wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani
  • Picha ya pamoja kati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (wa tatu kushoto mstari wa kwanza) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Ole Nasha (wa nne kulia mstari wa kwanza) pamoja na Watumishi wa Wizara walioshiriki mapokezi ya Mhe. Ole Nasha alipowasili Wizarani baada ya kuapishwa
  • Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akizungumza na Viongozi na Watumishi wa Wizara mara baada ya Wizarani baada ya kuapishwa
  • Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Agnela Nyoni wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani
  • Mhe. Prof. Kabudi akimtambulisha Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi kwa Naibu Waziri Mhe. Ole Nasha wakati wa mapokezi yake alipowasili Wizarani