Skip to main content
News and Events

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana kwa mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil

  • Picha ya pamoja kati ya Naibu Mawaziri na wajumbe wote wa Tanzania na Brazil
  • Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil, Mhe. Balozi Fernando Jose Marroni de Abreu (katikati) nae akizungumza wakati wa majadiliano ya kisiasa kati yake na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (hayupo pichani). Wengine kwenye picha ni Balozi wa Brazil nchini, Mhe. Carlos Alfonso Iglesias Puente (kushoto) na Mkuu wa Idara inayoshughulikia masuala ya Kaskazini na Mashariki mwa Afrika kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Brazil, Bw. Paulo Cypriano.
  • Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (katikati) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil, Mhe. Balozi Fernando Jose Marroni de Abreu (hayupo pichani) walipokutana kwa Majadiliano ya Kisiasa yaliyofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Aprili, 2018. Majadiliano hayo yalifanyika wakati wa ziara ya kikazi ya siku mbili ya Mhe. Balozi Fernando hapa nchini. Pamoja na mambo mengine walijadiliana kuhusu namna ya kuboresha mashirikiano ya kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili hususan katika eneo la biashara na uwekezaji. Pia Naibu Mawaziri hao walijadili namna ya kutekeleza kikamilifu Mradi wa Pamba kwenye eneo la Ziwa Victoria na matokeo ya kusainiwa kwa mkataba wa msamaha wa deni la Tanzania kwa Brazil pia lilijadiliwa. Aidha, Brazil wameahidi kushirikiana na Tanzania kwenye sekta ya afya hususan katika kupambana na maradhi ya Selimundu (Sircle-cell) na kwa upande wa Zanzibar watashirikiana katika afya ya mama na mtoto hususan kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga.
  • Mhe. Dkt. Susan Kolimba akimsikiliza kwa makini Mhe. Fernando de Abreu (hayupo pichani), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil wakati wa Majadiliano ya Kisiasa kati ya Tanzania na Brazil. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Salvator Mbilinyi (kulia)