Skip to main content
News and Events

NAIBU WAZIRI MKUU WA CHINA AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China na Mjumbe wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China, Mhe. Liu Gozhong, amewasili nchini kwa ziara ya siku tatu (3) kuanzia tarehe 22 hadi 24 Januari 2024 na kupokelewa na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri waNishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko (Mb.)

Ziara hii inafanyika ikiwa ni jitihada za makusudi kati ya Tanzania na China katika kuimarisha ushirikiano wa kihistoria na kidugu ulioasisiwa na kujengwa na waasisi wa mataifa hayo mawili mwaka 1964; Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na Mwenyekiti Mao Zedong wa China na kuimarishwa na awamu zote za uongozi zilizofuatia katika mataifa hayo mawili.

Pamoja na mambo mengine, akiwa nchini Mhe. Liu atatembelea; Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI ), Makumbusho ya Taifa, Shirika la Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kadhalika atatembelea eneo la makaburi ya wataalamu wakichina waliofariki wakati wa ujenzi wa reli ya TAZARA.

  • Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Liu Guozhong akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Mbarouk mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza zaia ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 22 hadi 24 Januari 2024. Aliyesimama kulia kwa Mhe. Balozi Mbarouk ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akifuatiwa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Khamis Mussa Omar
  • Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Liu Guozhong akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Samwel Shelukindo alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 22 hadi 24 Januari 2024
  • Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Liu Guozhong akisalimia wadau mbalimbali waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili nchini kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 22 hadi 24 Januari, 2024