Mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi za SADC wafunguliwa rasmi

Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja wa wajumbe mbalimbali waliohudhuria ufunguzi wa Mkutano wa 39 wa Kilele wa Wakuu hao wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa na Jumuiya ukipigwa. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine yaliyojiri katika mkutano huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa Jumuiya hiyo ambapo atahudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja 2019/ 2020 Mkutano huu unaofanyika kwa siku mbili utafikia tamati kesho tarehe 17 Agosti, 2019

Mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi za SADC wafunguliwa rasmi

  • Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akikabidhiwa uenyekiti na mwenyekiti anayemaliza muda wake Mhe. Hage Geingob Rais wa Namibia, wakati ufunguzi wa Mkutano wa kilele wakawaida wa Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi za SADC uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akifuatilia tukio hilo.
  • Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. David Cleopa Msuya (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. John Samuel Malecela (katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. faraji Kassidi Mnyepe wakifuatilia Mkutano wa 39 wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea jijini Dar Es Salaam,Katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere(JNICC)
  • Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaji Dkt. Ali Mohamed Shein (katikati) na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa,wakiwa wanafuatilia Mkutano wa 39 wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea jijini Dar Es Salaam,Katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere(JNICC)
  • Marais Wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi,Zanzibar pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali wakifuatilia Mkutano wa 9 wa Jumuiya hiyo unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JINCC) Dar es Salaam,Tanzania. Kutoka kulia ni Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamini William Mkapa akifuatiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akifuatiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya sita wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Aman Abeid Karume,akifuatiwa na Makamu wa Rais mstaafu wa awamu ya tatu Dkt Mohamed Gharib Bilali,akifuatiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi John Kijazi na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo.