MHESHIMIWA RAIS SAMIA AELEKEA NCHINI MAREKANI KWA ZIARA YA KIKAZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiagana na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es salaam wakati akielekea nchini Marekani kwa ziara ya kikazi. Akiwa nchini Marekani Mheshimiwa Rais Samia anatarajiwa kushiriki zoezi la uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour unaotarajiwa kufanyika tarehe 18 Aprili 2022 New York.