Skip to main content
News and Events

Mhe.LONDO AKUTANA NA UJUMBE WA WEF

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Dennis Londo (Mb.) tarehe 17 Agosti, 2024 amekutana na kuzungumza na Mkuu wa Agenda Ukanda wa Afrika wa Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum - WEF) Bw. Chido Munyati na Msaidizi wake Dr. Dieynaba Tandian na kuujadili kuhusu Ushiriki wa Tanzania katika Jukwaa la Uchumi Duniani litakaofanyika mwezi Januari, 2025.

Mhe. Londo ameainisha maeneo mahususi ambayo Tanzania imeyapa kipaumbele kwa ajili ya kujadiliwa katika Jukwaa hilo Ametaja hayo kuwa ni sekta ya Kilimo, Nishati, Mazingira na Mabadiliko ya Hali ya Hewa, Biashara, Viwanda na Utalii