MHE. BALOZI LIBERATA MULAMULA AFANYA ZIARA YA KIKAZI NCHINI AFRIKA KUSINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe. Grace Naledi Pandor walipokutana kujadili mambo ya kuendeleza ushirikiano baina Nchi hizi mbili. ****************************************************************************** ZIARA YA KIKAZI YA MHE. BALOZI LIBERATA MULAMULA, WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI NCHINI AFRIKA KUSINI 20 APRILI, 2021 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe. Grace Naledi Pandor kujadili mambo ya kuendeleza mashirikiano baina ya Jamhuri ya Afrika Kusini na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika majadiliano hayo Mhe Balozi Mulamula alieleza kuwa mahusiano kati ya Afrika Kusini na Tanzania ni ya kihistoria na yameendelea kuimarika tangu enzi a kupigania uhuru kwa nchi za kusini mwa Afrika. Tanzania ni nchi za mwamzo zilizofungua Ublozi wake hapa Afrika Kusini mwaka 1994. Kwa hivi sasa nchi zetu mbili zina mashirikiano ya ngazi ya juu yajulikanayo kama Bi-national Commission. Naye Mhe. Waziri Pandor alishukuru kwa ujio wa Mhe Balozi Mulamula na kwa kufika nchini Afrika Kusini na pia alieleza kuwa Jamhuri ya Afrika Kusini inathamini mashirikiano ya kihistoria kati ya nchi zetu mbili na hivyo kinachohitajika ni kuendeleza na kuimarisha mashirikiano ya kiuchumi na kisiasa tuliyonayo sasa hivi. Jamhuri ya Afrika Kusini inayo azma ya kushiriki kikamilifu kujenga makumbusho ya urithi (heritage museum) ya harakati za kupigania uhuru kusini mwa Afrika zenye chimbuko lake nchini Tanzania na vilevile kuonyesha juhudi za Tanzania katika harakati za kupigania uhuru na kwa nchi za kusini mwa Afrika. Mawaziri hao walijadili pia mchakato wa tathimini ya utekelezaji wa Bi-National Commission (BNC) ambapo kwa mwaka huu Afrika Kusini ndiyo itakuwa mwenyeji wa tathimini hiyo ambayo hujumuisha ngazi ya watedaji wakuu wa sekta mbalimbali wan chi hizi mbili, Mawaziri na huitimishwa na Waheshimiwa Marais wa nchi zote mbili. Tathimini hiyo hukutanisha wafanya biashara wa nchi zote mbili, kwa nia ya kukuza na kuendeleza biashara baina ya nchi hizi mbili. Mhe. Waziri Balozi Mulamula kabla ya kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, alikutana na watumishi wa ubalozi wa Tanzania Pretoria katika mkutano ulifanyika Ubalozini, Mhe. Waziri alipokea taarifa ya eneo la uwakilishi la Ubalozi ambalo linajumuisha Afrika Kusini, Botswana, Falme ya Lesotho na SADC. Taarifa hiyo ilieleza juhudi za Ubalozi katika kukuza mahusiano na nchi za eneo la uwakilishi, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa diplomasia ya uchumi, diplomasia ya siasa, wanadiaspora wa eneo la uwakilishi. Mhe. Waziri alipokea taarifa hiyo na kupongeza Ubalozi kwa kufanya kazi kwa ufanisi na weledi na kwa maslahi ya Taifa. Pamoja na mambo mengine, Mhe Waziri Mulamula alisema kwa vile huu ni Ubalozi wa kwanza ameutembelea tangu uteuzi wake kwa nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Hivyo ameutaka Ubalozi kuendela kufanya kazj kwa malengo, watumishi kujiwekea malengo binafsi ili kufanikisha malengo ya Ubalozi na hatimaye Ubalozi kuchangia malengo ya Wizara kwa ujumla. Aliupongeza Ubalozi kwa utunzaji mzuri wa majengo kwa fedha ndogo wanazozipata. Aidha, Mhe Waziri ameutaka Ublozi kuendeleza mahusiano na nchi za uwakilishi na Balozi zingine zilizopo katika nchi za uwakilishi na suala hili la kujenga mahusiano na watumishi wote na siyo Balozi pekee yake. Mhe. Waziri aliongeza kwa kusema kuwa Ubalozi uangalie fursa za mafunzo kwa wtumishi yaani watumishi kushiriki kozi fupi kwa nia ya kuwajengea uwezo watumishi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi Zaidi katika tasnia ya diplomasia. Mwisho, aliushukuru Ubalozi kwa mapokezi mazuri.
  • Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe. Grace Naledi Pandor.
  • Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini
  • Mazungumzo yakiendelea
  • Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akijadili jambo na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe. Meja Generali Gaudence Milanzi