Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aongoza Mkutano wa SADC - ORGAN
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ) Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Utatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi hiyo kwa njia ya mtandao katika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 11 Desemba, 2024.
Rais wa Romania, Mhe. Klaus Iohannis akizungumza kwenye hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa kwa heshima yake Ikulu Zanzibar.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. David Cleopa Msuya (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. John Samuel Malecela (katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. faraji Kassidi Mnyepe wakifuatilia Mkutano wa 39 wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea jijini Dar Es Salaam,Katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere(JNICC)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais wa Romania, Mhe. Klaus Iohannis Ikulu Zanzibar