Mabalozi wakabidhiwa Viwanja vya Ofisi Jijini Dodoma
Mabalozi wakabidhiwa Viwanja vya Ofisi Jijini Dodoma
Baadhi ya Mabalozi wakimsikiliza Bw. Godwin Kunambi na wataalam wake (hawapo pichani) wakielezea michoro mbalimbali ya miundombinu kwenye eneo hilo la wanadiplomasia. (Pichani juu na chini
Mkurugenzi wa iliyokuwa Manispaa ya Dodoma na sasa Jiji la Dodoma Bw. Godwin Kunambi akiwaonesha Mabalozi ramani ya Mji wa Serikali ambayo ndani yake kuna viwanja vya kujenga ofisi za kibalozi jijini humo. Viwanja hivyo viligawiwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mapema mwaka huu kwa nia ya kuharakisha na kuhamasisha Jumuiya ya Kimataifa kujenga ofisi na makazi yao ya uwakilishi kwenye Makao Makuu ya nchi, Dodoma. Zoezi hilo la ugawaji wa viwanja liliratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma siku moja kabla ya mabalozi hao kuhudhuria sherehe za Muungano tarehe 26 Aprili 2018.
Baadhi ya wanadiplomasia wakiwa na nyuso za furaha kwenye kiwanja cha Ubalozi wa Zambia pamoja na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje. Kiwanja hicho cha mfano kilisafishwa kwa lengo la kuonesha ukubwa wa viwanja hivyo vilivyotolewa na Rais Magufuli ili kufanikisha uhamiaji wa Balozi hizo Jijini Dodoma, makao makuu ya nchi.