Skip to main content
News and Events

ISRAEL KUSAIDIA SEKTA YA AFYA NCHINI

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bibi Dkt. Otilia Flavian Gowelle pamoja na Naibu Balozi wa Israel nchini, Mhe. Michael Baruch Baror wakiweka saini Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika sekta ya Afya kati ya Tanzania na Israel. Makubaliano hayo yataanza kwa kuijengea uwezo hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma ambapo Israel itasaidia ujenzi wa Kitengo cha dharua na mifupa pamoja na ujenzi wa Kitengo cha kisasa cha wagonjwa mahututi (ICU).