Skip to main content
News and Events

WAZIRI WA MAMBO YA NJE ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI WA VIETNAM


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiweka saini katika kitabu cha maombolezo cha ubalozi wa Vietnam hapa nchini kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Rais wa Taifa hilo Jenerali Le Duc Anh aliyefariki April 22,2019, wa pili kutoka kushoto ni Balozi wa Vietnam hapa nchini Mhe. Nguyen Doanh na watatu kutoka kulia ni Mke wa Balozi Doanh pamoja na maafasia ubalozi huo wakishuhudia tukio hilo. 

Mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo Prof. Palamagamba John Kabudi ametoa pole kwa wananchi kupitia kwa Balozi wa Vietnam hapa nchini  nakuelezea kuwa Jamhuri ya Kisoshalisti ya watu wa Vietnam na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zina uhusiano wa muda mrefu na wa miaka mingi tangu enzi za Jamhuri ya watu wa Vietnam wakipigania Uhuru wao kutoka kwa Mareakani na Ufaransa.

Tukio hilo limefanyika katika Ubalozi wa Vietnam uliopo jijini Dar es Salaam leo tarehe 4, Mei 2019
 

  • Prof. Palamagamba John Kabudi akiagana na Balozi Doanh mara baada ya kumaliza tukio hilo.Prof. Palamagamba John Kabudi akiagana na Balozi Doanh mara baada ya kumaliza tukio hilo.
  • Prof. Palamagamba John Kabudi akielezea jambo mara baada ya kuweka saini kwenye kitabu cha maombolezoProf. Palamagamba John Kabudi akielezea jambo mara baada ya kuweka saini kwenye kitabu cha maombolezo
  • Mazungumzo yakiendelea.Mazungumzo yakiendelea.