Skip to main content
News and Events

WAZIRI WA DENMARK ATEMBELEA HOSPITALI YA CCBRT

Waziri wa Ushirikiano na Maendeleo wa Denmark Mhe. Dan Jorgensen ametembelea Hospitali ya CCBRT ya jijini Dar es salaam na kujionea jinsi hospitali hiyo inavyoendesha shughuli zake kwa Watanzania.

Mhe. Jorgensen ametembelea sehemu zinazotoa Huduma ya matibabu kwa kına mama walioathiriwa na ugonjwa wa Fistula, sehemu ya uundwaji wa viungo bandia na mazoezi kwa watumiaji wa viungo hivyo bandia , urekebishaji wa uoni kwa watoto waliozaliwa na uoni hafifu au bila macho na wodi ya kijifungulia.

Mhe. Jorgensen ametembelea hospitali hiyo ya CCBRT ili kujionea jinsi fedha zinazotolewa na Serikali ya Denmark zinavyowezesha utoaji wa huduma bora kwa Watanzania

  • Waziri wa Ushirikiano na Maendeleo wa Denmark Mhe. Dan Jorgensen akisikiliza maelezo jinsi mguu bandia unavyotengenezwa katika Hospitali ya CCBRT ya jijini Dar es salaam alipoitembelea kujionea jinsi hospitali hiyo inavyoendesha shughuli zake kwa Watanzania.
  • Waziri wa Ushirikiano na Maendeleo wa Denmark Mhe. Dan Jorgensen akiangalia baadhi ya bidhaa zilizotengenezwa na wagonjwa katika Hospitali ya CCBRT jijini Dar es salaam alipoitembelea kujionea jinsi hospitali hiyo inavyoendesha shughuli zake kwa Watanzania.