Skip to main content
News and Events

WAZIRI MULAMULA AFANYA MAZUNGUMZO NA MSAIDIZI MAALUM WA RAIS WA MAREKANI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana kwa mazungumzo na Msaidizi Maalum wa Rais wa Marekani na Mkurugenzi Mwandamizi katika Baraza la Usalama la Taifa Bi. Dana L. Banks.

Mazungumzo hayo yamelenga juu ya kuwawezesha wanawake kuhusu biashara ili kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na mikakati ya kupambana na ugaidi.

  • Mazungumzo yakiendelea
  • Bi. Dana L. Banks Msaidizi Maalum wa Rais wa Marekani na Mkurugenzi Mwandamizi katika Baraza la Usalama la Taifa akiwa katika mazungumzo na Mhe. Balozi Liberata Mulamula Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hayuko pichani)