Waziri Mkuu atembelea Mji wa Serikali uliopo Mtumba, Dodoma
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akizungumza alipotembelea Jengo la Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki linalojengwa kwenye Mji wa Serikali uliopo Mtumba jijini Dodoma. Pamoja na mambo mengine, Mhe. Waziri Mkuu alizipongeza baadhi ya Wizara kwa kukamilisha majengo ya Ofisi zao na kuzitaka Wizara zote kuhakikisha zinakamilisha hatua za mwisho za ujenzi huo ikiwa ni pamoja na kusawazisha maeneo na kuweka miundombinu muhimu kama maji na umeme kabla ya tarehe 15 Aprili 2015. Aidha, aliziagiza Taasisi kama TANESCO, TARULA na DUWASA kukamilisha kuweka huduma hizo muhimu za umeme, maji na barabara kwenye mji huo. Tayari Wizara 20 zimekamilisha majengo ya ofisi zao kwa zaidi ya asilimia 98. Wengine katika picha ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Anisa Mbega (kulia) na Katibu wa Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Kutaribu mpango wa Serikali kuhamia Dodoma, Bw. Meshack Bandawe (katikati). Ziara hiyo imefanyika tarehe 27 Machi 2019
Baadhi ya mafundi wanaoendea na ujenzi wa jengo la ofisi za Wizara Mtumba wakiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Deus Kaganda wakati wa ziara ya Waziri Mkuu kwenye Mji wa Serikali uliopo Mtumba
Mhe. Waziri Mkuu akikagua moja ya chumba cha ofisi katika jengo la Wizara lililopo Mtumba
Mhe. Waziri Mkuu akitoa maelekezo kwa Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Mbega alipotembelea jengo la Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki lililopo Mtumba jijini Dodoma. Pamoja na mambo mengine ameitaka Wizara kuharakisha usawazishaji