WAZIRI KOMBO AWASILI MAKAO MAKUU YA EAC ARUSHA KUSHIRIKI MKUTANO WA 46 WA MAWAZIRI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thatib Kombo akiwasili katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha leo tarehe 28 Novemba 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 46 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya hiyo.
Mkutano wa Mawaziri unafanyika kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa EAC utakaofanyika tarehe 29 na 30 Novemba 2024.
Mhe. Balozi Kombo anaongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo wa Mawaziri.