WAJUMBE WA KAMATI YA NUU WATEMBELEA MIRADI YA KIKANDA YA EAC
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Vita R. Kawawa, wameitaja Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kama Jumuiya yenye maono na inayatafsiri kivitendo maono yake.
Wameeleza hayo wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya kikanda ya Barabara ya EAC iliyofanyika katika mikoa ya Dodoma, Manyara na baadaye Arusha kuanzia tarehe 02 hadi 04 Septemba 2022.
Ziara hiyo iliyoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ilitoa fursa kwa wajumbe wa Kamati ya NUU kujionea baadhi ya miradi ya Jumuiya na namna Tanzania inavyoshirikiana na Sekretarieti ya EAC na nchi wanachama kutekeleza miradi hiyo, kuanzia kufanya uchambuzi yakinifu na baadaye kutafuta fedha za utekelezaji.
Wajumbe walielezwa kuwa Tanzania imepakana na nchi tano za EAC ambazo ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na katika nchi zote hizo kuna miradi ya barabara ya kuiunganisha Tanzania na nchi hizo ambayo baadhi yao imekamilika, mingine ipo katika hatua za ujenzi na mingine inatafutiwa fedha ili iweze kutekelezwa.
Miradi michache ambayo ipo katika ujenzi ni pamoja na barabara ya kutoka Kabingo, Kasulu hadi Manyovu yenye urefu wa kilomita 260 inayounganisha Tanzania na Burundi. Barabara ya kutoka Tanga, Pangani, Saadan hadi Bagamoyo yenye urefu wa kilomita 256 inayounganisha Tanzania na Kenya. Ujenzi wa barabara hiyo utajumuisha pia daraja la Pangani la mita 500.
Kwa upande wa Tanzania na Uganda, kuna mradi wa barabara ya Mutukula, Kiyaka, Kasulu hadi Benako yenye urefu wa kilomita 124 na Bugene, Burigi, Chato hadi Kasulo yenye urefu wa kilomita 68.
Wakikagua barabara ya kikanda ya Arusha, Namanga, Ath River pamoja na barabara ya mzunguko ya Arusha, wajumbe wlielezea namna ujenzi wa barabara hizo unvyounganisha nchi wanachama wa EAC na kuchochea biashara, muingiliano wa watu na hatimaye kuimarisha mtangamano wa EAC.
Walisisitiza umuhimu wa nchi zote wanachama kuwa wamoja bila kujali mipaka ya nchi zao ili kwa pamoja waweze kutafutia ufumbuzi wa changamoto zinazotokana na utekelezaji wa miradi hiyo.
Wajumbe wa Kamati hiyo ambao pia walitembelea Kituo cha Pamoja cha Mpakani cha Namanga, walisikiliza mada kutoka kwa Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota. Mada hiyo pamoja na mambo mengine, ilieleza miradi mingine inayotekelezwa kwa uratibu wa EAC katika sekta za usafiri wa anga, reli, majini; hali ya hewa na nishati katika nchi wanachama wa Jumuiya.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) wakifuatilia kwa makini mada kuhusu utekelezaji wa miradi ya kikanda ya miundombinu ya EAC iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala, Mhandisi Steven Mlote akiongea jambo wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) ilipotembelea Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mshariki jijini Arusha kabla ya kuanza kutembelea miradi ya miundombinu ya EAC inayotekelezwa mkoani humo. Mwingine katika picha ni Mwenyekiti wa Kamati ya NUU, Mhe. Vita R. Kawawa
Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa miradi ya kikanda ya miundombinu ya EAC kwa wajumbe wa Kamati ya NUU jijini Arusha.
Mjumbe wa Kmati ya NUU, Mhe. Janeth Masaburi akichangia jambo kuhsu utekelezaji wa miradi ya kikanda ya miundombinu ya EAC
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya NUU, Mhe. Vicent Mbogo akichangia hoja baada ya kuwasilishwa mada kuhusu utekelezaji wa miradi ya kikanda ya miundombinu ya EAC
Mwenyekiti wa Kamati ya NUU, Mhe. Vita R. Kawawa akichangia hoja baada ya kuwasilishwa mada kuhusu utekelezaji wa miradi ya kikanda ya miundombinu ya EAC
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) wakifuatilia kwa makini mada kuhusu utekelezaji wa miradi ya kikanda ya miundombinu ya EAC iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Lungido, Bw. Kamana Juma Simba akitambulisha ujumbe wa Wilaya yake ulioshiriki katika ziara ya wajumbe wa Kamati ya NUU katika Kituo cha Pamoja cha Mpakani cha Namanga
Meneja wa Mamlaka ya Mapato wa Mkoa wa Arusha, Bw. Paul Kamukulu akifafanua jambo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Kituo cha Pamoja cha Mpakani cha Namanga kwa wajumbe wa Kamati ya NUU walipotembelea kituo hicho tarehe 03 Septemba 2022.
Mwenyekiti wa Kamati ya NUU, Mhe. Vita R. Kawawa akipokelewa na watumishi wa Kituo cha Pamoja cha Mpakani cha Namanga, mara baada ya kuwasili na kamati yake katika kituo hicho kwa ajili ya kuangalia utendaji wa Kituo.
Waheshimiwa Wajumbe wa Kamati ya NUU na wajumbe wengine wakisikiliza mada kuhusu utekelezaji wa miradi ya kikanda ya miundombinu ya EAC
Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mahariki, Bw. Justin Kisoka akijumuika na wajasiriamali wanaofanya biashara maeneo ya kuzunguka Kituo cha Pamoja cha Mpakani cha Namanga
Mjumbe wa Kamati ya NUU, Bw. Cosato Chumi akijumuika na wajasiriamali wanaofanya biashara maeneo ya kuzunguka Kituo cha Pamoja cha Mpakani cha Namanga
Wajumbe wa Kamati ya NUU wakisikiliza majumuisho ya ziara yao kutoka kwa Afisa kutoka Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii, Bw. Imail Abdalla
Afisa kutoka Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii, Bw. Imail Abdalla akifanya majumuisho ya ziara ya Kamati ya NUU katika miradi ya miundombinu ya EAC iliyofanyika kuanzia tarehe 02 hadi 04 Septemba 2022
Meneja wa Mamlaka ya Mapato wa Mkoa wa Arusha, Bw. Paul Kamukulu akisoma taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Kituo cha Pamoja cha Mpakani cha Namanga kwa wajumbe wa Kamati ya NUU
Picha ya pamoja