Skip to main content
News and Events

WAATALAM WA SEKTA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA, UTAMADUNI NA MICHEZO KUTOKA NCHI ZA EAC WAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM

Wataalam wa Sekta wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Utamaduni na Michezo kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamekutana leo tarehe 18 Juni 2024 jijini Dar es Salaam katika kikao cha maandalizi ya Mkutano wa Saba wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Utamaduni na Michezo unaotarajiwa kufanyika tarehe 22 Juni, 2024.

Mkutano wa ngazi ya wataalam ambao utafuatiwa na ule wa Makatibu Wakuu, pamoja na masuala mengine, unapitia na kujadili utekelezaji wa maagizo ya mikutano iliyopita, na hatua za utekelezaji wa miradi na programu za Elimu, Sayansi na Teknolojia, Utamaduni na Michezo. 

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano Ngazi ya Wataalam umeongozwa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhandisi Abdillah Mataka ambaye ameambatana na Wataalamu Waandamizi kutoka sekta ya  Elimu, Sayansi na Teknolojia, Utamaduni na Michezo.