Skip to main content
News and Events

TANZANIA - ZAMBIA WAJADILI MASUALA YA USHIRIKIANO

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zambia zinakutana jijini Lusaka, Zambia kujadili masuala ya ushirikiano yaliyokubaliwa baina ya nchi hizo mbili.

Majadiliano hayo yanafanyika katika ngazi ya Wataalam ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa Kumi wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia unaofanyika kuanzia tarehe 11 hadi 14 Oktoba 2022.

Mkutano wa Wataalam utafuatiwa na mkutano ngazi ya Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 12 Oktoba 2022 na kumalizika na mkutano ngazi ya Mawaziri utakaofanyika tarehe 14 Oktoba 2022 jijini Lusaka Zambia

Mkutano huu unajadili na kutathimini utekelezaji wa maazimio katika sekta mbalimbali za ushirikiano zilizokubaliwa katika mkutano wa tisa uliofanyika tarehe 25 hadi 26 Februari 2016 jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Maeneo ya ushirikiano ni pamoja na; Siasa, Ulinzi na Usalama, Mambo ya Nje, Uhamiaji, Fedha na Uchumi, Sheria, Nishati, Habari na Mawasiliano, Kilimo, Miundombinu, Uchukuzi na Usafirishaji, Elimu, Sayansi na Teknolojia, Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Utalii, Kilimo, Uvuvi, Mazingira na Maliaasili, Afya, Elimu, Vijana na Michezo na jinsia.

Mkutano huu unafanyika kufuatia maagizo ya Marais wa pande zote mbili wakati wa ziara ya kiserikali ya Rais wa Jamhuri ya Zambia nchini Tanzania, Mhe. Hakainde Hichilema mapema mwezi Agosti 2022.

  • Mchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Clementine Msafiri akifuatilia majadiliano.
  • Afisa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki - Ofisi ya Zanzibar, Bi. Asya Ali Hamdani akifuatilia mkutano huo.
  • Kutoka kushoto ni Mkuu wa Utawala na Fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia, Bw. Humphrey Shangarai na Afisa Ubalozi Bw. Sunday Iddi wakifuatilia majadiliano.
  • Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia majadiliano, kulia Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Brig. Jen. Michael M. Mumanga na kushoto ni Afisa Mambo ya Nje Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Makamba D. Makamba.
  • Kutoka kushoto ni Kamishna Msaidizi Idara ya Uchambuzi wa Sera katika Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. William Mhoja na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mtangamano wa Biashara katika Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara wakifuatilia majadiliano katika mkutano wa wataalam
  • Mwenyekiti mwenza wa mkutano ngazi ya wataalamu Bw. Lubasi Mugandi akiongoza ujumbe wa Zambia katika Mkutano wa Kumi wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia - ngazi ya Wataalam unaofanyika leo tarehe 11 Oktoba 2022 jijini Lusaka Zambia.