Skip to main content
News and Events

RAIS WA SENEGAL AWASILI NCHINI KUHUDHURIA AGRF 2023

Rais wa Jamhuri ya Sénégal Mhe.Macky Sall amewasili nchini kuhudhuria Mkutano wa Mifumo ya Chakula Afrika unaofanyika nchini kuanzia tarehe 5-8 Septemba 2023.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam Mhe. Sall alilakiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki.

Mhe.Sall  ni miongoni mwa Wakuu wa Nchi na Serikali, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa na Marais na Mawaziri Wakuu wastaafu kutoka barani Afrika wanaohudhuria mkutano huo mkubwa unaojadili mifumo ya chakula duniani