Skip to main content
News and Events

RAIS WA ROMANIA AWASILI NCHINI

Rais wa Romania, Mheshimiwa Klaus Iohannis, amewasili nchini kwa ziara ya Kitaifa kuanzia leo tarehe 16 hadi 19 Novemba 2023 kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere amepokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki (Mb.)

Lengo la ziara hiyo ni pamoja na kushawishi uwekezaji zaidi na kuvutia watalii wengi kutoka nchini Romania.

Aidha katika mazungumzo rasmi yatakayofanyika tarehe 17 Novemba 2023 Rais huyo na mwenyeji wake watajadili namna bora ya kukuza na kuimarisha ushirikiano kati sekta za elimu, afya, kilimo nishati na madini.

Kabla ya kuondoka nchini tarehe 19 Novemba 2023 Rais wa Romania atapata fursa ya kwenda Zanzibar ambapo atazungumza na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi na kutembelea mji mkongwe ambao ni moja kati ya vivutio vikubwa vya utalii duniani

  • Meza Kuu wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kwenye hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais wa Romania, Mhe. Klaus Iohannis Ikulu Zanzibar
  • Rais wa Romania, Mhe. Klaus Iohannis akizungumza kwenye hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa kwa heshima yake Ikulu Zanzibar.Rais wa Romania, Mhe. Klaus Iohannis akizungumza kwenye hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa kwa heshima yake Ikulu Zanzibar.
  • Rais wa Romania, Mheshimiwa Klaus Iohannis akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samuel Shelukindo alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam
  • Rais wa Romania, Mheshimiwa Klaus Iohannis akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki (Mb.)  alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es SalaamRais wa Romania, Mheshimiwa Klaus Iohannis akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki (Mb.) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam
  • Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. David Cleopa Msuya (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. John Samuel Malecela (katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. faraji Kassidi Mnyepe wakifuatilia Mkutano wa 39 wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea jijini Dar Es Salaam,Katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere(JNICC)