RAIS PEREIRA AFUNGUA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA UMOJA WA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU RASMI JIJINI ARUSHA
Rais wa Jamhuri ya Cabo Verde Mhe. José Maria Pereira Neves, amezitaka nchi za Afrika kuimarisha demokrasia na Utawala bora ili kuepuka kujirudiarudia kwa makosa yaliyotokana na nchi kutawaliwa na wakoloni na kusababisha baadhi yake kuendelea kudai fidia hadi sasa.
Rais Neves, akihutubia kama mgeni rasmi katika Ufunguzi wa Mwaka Mpya wa Mahakama ya Umoja wa Afrika ya Haki za Bianadamu, ametoa angalizo dhidi ya migogoro inayoendelea kutokea Barani Afrika inayorudisha maendeleo ya Jamii kubwa, sababu ikionekana kutokuzingatiwa kwa haki za bianadamu na Uongozi Bora.
“Naipongeza Mahakama ya umoja wa Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kwa kuchagua kaulimbiu nzuri ya ulipaji Fidia kuendeleza haki kwa watu wa Afrika hata hivyo zoezi la ulipaji fidia ni zaidi ya ulipwaji wa fidia, kwa kuwa inahusiasha mambo mbalimbali makubwa ikiwemo kuponya majeraha ya kihistoria Haitoshi kuishi katika kulaani na kukemea kwa maneno, miaka ijayo kuna vizazi vitakuja kudai fidia kwa migogoro yetu wenyewe na sio wakoloni.” Alisema Mhe. Pereira Neves
Awali Rais wa Mahakama ya Umoja wa Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Mhe. Jaji Imani D. Aboud akihutubia kwenye ufunguaji wa mwaka mpya wa Mahakama hiyo alieza umuhimu wa kauli mbiu waliochagua umezingatia hali halisi ya dhamira na Mahakama hiyo katika kuhakikisha watu walio pitia na wanaopitia hali ya ukandamizaji wa Haki za Binadamu wanalipwa fidia.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo majaji, viongozi kutoka kwenye Taasisi za Utetezi na Utoaji Haki za Binadamu barani Afrika. Aidha, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imewakilishwa na Mhe. Dennis L. Londo (Mb.); Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye amemwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabiti Kombo (Mb.). Vilevile, Mhe. Londo aliambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Musa.
Ufunguzi wa Mwaka Mpya wa Mahakama ya Umoja wa Afrika ya Haki za Bianadamu, Umefanyika katika Makao Makuu ya Mahakama hiyo yaliyopo jijini Arusha tarehe 03 Februari, 2025.