Pumzika kwa Amani Mhe Dkt John Pombe Magufuli
Uongozi, Menejimenti pamoja na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika mashiriki umepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021 Dar es Salaam.
Uongozi na Wizara kwa ujumla unaungana na Watanzania wote katika maombolezo ya msiba huu mzito kwa Taifa letu.