Prof. Kabudi akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akisaini mkataba wa msaada wa shilingi bilioni sitini bila ya masharti yeyote pembeni yake ni Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la Misaada ya Maendeleo la China Bw. Zhou Liujun,akisaini kwa niaba ya serikali ya China. Zoezi hilo limefanyika Beijing,China. June 24, 2019.
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akibadilishana nyaraka na Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la Misaada ya Maendeleo la China Bw. Zhou Liujun, mara baada ya kusaini nyaraka hizo. Zoezi
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) na ujumbe wake akiwa kwenye mkutano pamoja na mwenyeji wake ambaye ni Waziri wa mambo ya nje wa China na na Mjumbe wa Baraza la Taifa Mhe. Wang Yi na ujumbe wake.
Bw. Zuberi Kachingwe Afisa Usafirisahaji, IKULU,(katikati) akitoa maelezo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akikagua magari yatakayotumiwa na viongozi na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kujiridhisha juu ya matayarisho ya mapokezi kwa ajili ya mkutano huo utakaofanyika Dar es Salaam,Tanzania. Kulia ni Afisa Usafirishaji Msaidizi Bw. Athumani Natepe. August 8, 2019.