Skip to main content
News and Events

Prof. Kabudi akutana na Mabalozi wa Nchi za SADC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) waliopo hapa nchini.


Katika mazungumzo hayo Prof. Kabudi amewafahamisha hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya Mkutanao ya wakuu wa nchi na Serikali wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliyopangwa kufanyika nchini mwezi Agosti 2019 


Kwa upande wa waheshimiwa Mabalozi hao walifurahishwa kwa hatua ya maandalizi iliyofikiwa, na kuelezea furaha yao kuhusu uwamuzi wa Serikali kuwashirikisha mapema katika maandalizi hayo.

  • Sehemu ya Mabalozi wa Nchi za Afrika na wanachama wa Jumuiya ya SADC wakimsikiliza Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani)Sehemu ya Mabalozi wa Nchi za Afrika na wanachama wa Jumuiya ya SADC wakimsikiliza Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani)
  • Sehemu nyingine ya watumishi kutoka Balozi za Afrika zilizopo nchiniSehemu nyingine ya watumishi kutoka Balozi za Afrika zilizopo nchini
  • Prof. Palamagamba John Kabudi akifafanua jambo kwa Waheshimiwa Mabalozi alipokutana naoProf. Palamagamba John Kabudi akifafanua jambo kwa Waheshimiwa Mabalozi alipokutana nao
  • Balozi wa Afrika Kusini Mhe. Thamsanga Mseleku akielezea jambo katika mkutano na Waziri Prof. Palamagamba John KabudiBalozi wa Afrika Kusini Mhe. Thamsanga Mseleku akielezea jambo katika mkutano na Waziri Prof. Palamagamba John Kabudi
  • Mkutano ukiendelea.Mkutano ukiendelea.