Skip to main content
News and Events

NAIBU WAZIRI MHE. COSATO CHUMI APOKEA NAKALA HATI YA UTAMBULISHO KUTOKA KWA BALOZI MTEULE WA UINGEREZA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. David Cosato Chumi (Mb.) amepokea nakala ya Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Uingereza Mhe Marianne Young katika tukio lililofanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam 

Akizungumza baada ya kupokea nakala ya Hati hiyo , Mhe. Chumi amempongeza Mhe. Young kwa kupewa jukumu hilo na kumuahidi kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itakuwa Karibu naye na kumpa ushirikiano  muda wote wa uwakilishi wake hapa nchini ili kumuwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Naye Mhe. Balozi Young ameishukuru Serikali ya Tanzania na ameahidi kuendeleza mazuri yote yaliyoanzishwa na mtangulizi wake na kuongeza kuwa  yuko tayari kuibua masuala mengine mapya ya ushirikiano kwa maslahi ya pande zote.

Tanzania na Uingereza zimekuwa zikishirikiana katika maeneo ya uhusiano wa kidiplomasia, elimu, afya, utalii, biashara na uwekezaji