Skip to main content
News and Events

MASHINDANO YA SADC KWA WAANDISHI WA HABARI KWA MWAKA 2021

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

MASHINDANO YA SADC KWA WAANDISHI WA HABARI KWA MWAKA 2021

Dodoma, 15 Oktoba 2020

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuufahamisha umma kuwa Sekretariati ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imetangaza kuanza rasmi kwa mashindano ya waandishi wa habari kwa mwaka 2021 (2021 SADC Media Awards Competition). Shindano hili litakuwa katika Makundi manne (4) yafuatayo; picha, uchapishaji, runinga na radio. 

Washindi wa shindano hili, linalohusisha washiriki kutoka Nchi zote Wanachama wa SADC watatangazwa kwenye Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika mwezi Agosti, 2021 ambapo watapewa zawadi na vyeti. 

Wizara inapenda kuwahimiza Waandishi wa Habari watakaokidhi vigezo kujaza na kuwasilisha fomu za maombi ya kushiriki katika shindano hili, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kabla ya tarehe 28 Februari 2021. Kwa taarifa zaidi na kupata fomu za maombi za kushiriki shindano, taratibu na masharti ya kuzingatia, tafadhali tembelea https://www.sadc.int/media-centre/competitions-and-awards/media-awards/

 

Imetolewa na:

Emmanuel Buhohela

Mkurugenzi,

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.

Downloads File: