Katibu Mkuu akutana na Watumishi wa Wizara
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akizungumza kwenye kikao cha kwanza na Watumishi wote wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani) tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo. Pamoja na mambo mengine, Dkt. Mnyepe aliwataka Watumishi wa Wizara kufanya kazi kwa kufuata miongozo na kutekeleza majukumu yao kwa bidii, weledi na uzalendo. Mkutano huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo kwenye Ofisi za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali uliopo jijini Dodoma tarehe 21 Desemba 2018. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Ramadhan M. Mwinyi (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Savera Kazaura.