Skip to main content
News and Events

Dkt. Ndumbaro aanza na Makampuni 41

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), akizungumza na waandishi wa Habari juu ya ujio wa Ujumbe mkubwa wa wawekezaji kutoka Ubelgiji, katika mkutano huo na waandishi wa habari Dkt. Ndumbaro aliwaeleza waandishi kuwa "Ushirikiano wetu na Ubelgiji umekuwa mkubwa sasa na kupitia Ubalozi wetu nchini humo umewezesha ujio huu ambapo leo mchana tunawapokea rasmi wangeni hao na tuna imani utafungua ajira mbalimbali zikiwemo za moja kwa moja". hivyo watanzania wachangamkie fursa zitakazoletwa na wawekezaji hao. 

Aidha ujumbe huo wa wawekezaji utakuwepo nchini kuanzia Tarehe 24 mpaka 28 Octoba 2018, ambapo wawekezaji hao wanataraijiwa kufanya Kongamano kubwa la biashara hapo kesho katika Hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar es Salaam 

  • Balozi wa Ubelgiji nchini Mhe. Peter VanAcker naye akizungumza kwenye mkutano huo na waandishi wa Habari
  • Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya Bw. Jestas Nyamanga akifafanua jambo wakati wa mazungumzo hayo.