Skip to main content
BALOZI MULAMULA AKUTANA NA NAIBU KATIBU MKUU WA UN
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiendelea na mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe, Amina Mohammed (mwenye kilemba). Wengine wanaofuatilia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi, Robert Kahendaguza; Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Balozi Mindi Kasiga na Afisa Dawati, Bi. Gloria Ngaiza.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe, Amina Mohammed (mwenye kilemba) wakifurahia jambo wakati wa mazungumzo.yao yaliyofanyika jijini Kigali, Rwanda.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi, Robert Kahendaguza akiwa katika mazungumzo ya utangulizi na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe, Amina Mohammed (mwenye kilemba). Mwingine katika picha ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Balozi Mindi Kasiga.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe, Amina Mohammed jijini Kigali, Rwanda wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola. Mazungumzo hayo yaliangazia masuala makuu matatu ambayo ni mikutano inayoandaliwa na Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu, Usalama wa Chakula na namna dunia itakavyojikwamua kiuchumi baada ya UVIKO-19.