Skip to main content
News and Events

BALOZI MBUNDI AONGOZA KIKAO CHA NDANI CHA MAANDALIZI YA MKUTANO WA MAKATIBU WAKUU WA EAC

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki-anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi ameongoza kikao cha ndani cha maandalizi ya mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kilichofanyika tarehe 25 Juni, 2024 jijini Arusha.

Kikao hicho cha ndani pamoja na masuala mengine kimepitia agenda, taarifa na maagizo mbalimbali yaliyotolewa katika mikutano iliyopita ili kuona hali ya utekelezaji sambamba na kujenga msimamo wa Nchi katika masuala yenye maslahi mapana kwa ustawi wa watanzania na Taifa kwa ujumla.

Mkutano huo wa Makatibu Wakuu wa EAC utafanyika tarehe 26 na 27 Juni, 2024 ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa 45 wa Kawaida wa  Baraza la Mawaziri utakaofanyika tarehe 28 Juni 2024 jijini Arusha.