Balozi. Mbarouk Nassoro Mbarouk kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan amepokea ujumbe maalum wa Rais wa Indonesia
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Mbarouk (Mb) kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amepokea Ujumbe Maalumu wa Rais wa Indonesia, Mhe. Joko Widodo uliowasilishwa kwake na Mjumbe Maalum wa Rais Widodo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Indobesia, Mhe. Pahala M. Mansury. Ujumbe huo ulipokelewa leo Julai 20, 2024 katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam