Skip to main content
News and Events

BALOZI IBUGE ATOA SOMO KWA WABUNGE KUHUSU DIPLOMASIA NA ITIFAKI

Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akitoa somo kwa Wabunge huku Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Akson na Katibu wa Bunge Bw. Stephen Kigaigai wakimsikilizaa.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, ametoa somo la Diplomasia na Itifaki kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Balozi Ibuge ametoa somo hilo tarehe 16 Novemba 2020 katika semina iliyofanyika katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

Katika Semina hiyo, Balozi Brig. Gen. Ibuge aliwaeleza Wabunge hao kwa ujumla kuhusu dhana ya Itifaki; Itifaki ya Viongozi wa Kitaifa; Itifaki katika mawasiliano ya Viongozi; Itifaki ya mawasiliano rasmi na Balozi zilizopo hapa nchini.

Dhana nyingine ni pamoja na Itifaki ya upeperushaji Bendera na mipaka yake; Itifaki ya mavazi kwa viongozi pamoja na mambo mengine kuhusu Itifaki kwa Wabunge na Viongozi wote nchini.

Semina hiyo ililenga kuwajengea Wabunge uelewa mpana zaidi kuhusu masuala ya Diplomasia na Itifaki ikiwa ni moja ya masuala muhimu ya kuyafahamu kama zilivyo sheria na taratibu mbalimbali ambazo kwa namna moja ama nyingine watakutana nazo katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya Kibunge.

.

  • Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiendelea kutoa mada kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania eneo la Itifaki na Diplomasia.Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiendelea kutoa mada kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania eneo la Itifaki na Diplomasia.
  • Waheshimiwa  Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.wakifuatilia mada  ya Diplomasia na ItifakiWaheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.wakifuatilia mada ya Diplomasia na Itifaki