Skip to main content
News and Events
Press Release

XI JINPING AMLILIA HAYATI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

XI JINPING AMLILIA HAYATI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI.

Dodoma, 23 Machi 2021

Rais wa Jamhuri ya Watu wa China XI Jinping amemuandikia barua ya Kiserikali Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwanza kumpa pole kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na pili kumpongeza kwa kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika barua hiyo Rais XI Jinping amesema, amepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, na kwa niaba ya Serikali, Watu wa China na yeye binafsi anatoa salamu za rambirambi kwa familia, Serikali na Watanzania kwa ujumla kufuatia msiba huo. Amemuelezea Dkt. Magufuli kama kiongozi maarufu kwa Tanzania na Afrika ambaye aliwaongoza watu wa Tanzania kulinda hadhi ya Nchi yao dhidi ya kuingiliwa na mataifa ya kigeni na kuipatia maendeleo yanayoendana na hali halisi ya Tanzania. Ameongeza kuwa Dkt. Magufuli ametoa mchango chanya katika kuendeleza urafiki kati ya China na Tanzania pia China na Afrika.

“Kifo cha Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ni pigo kwa Watanzania na pia China imempoteza rafiki wa kweli” amesema XI Jinping.

China inajivunia urafiki wa muda mrefu na Tanzania na itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukuza urafiki huo katika kiwango cha juu kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.

 

Imetolewa na:

Emmanuel Buhohela

Mkurugenzi, Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali