Wizara ya Mambo ya Nje yashiriki uzinduzi wa mji wa serikali
Leo tarehe 13 Aprili, 2019, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imeshiriki katika hafla ya kuuzindua Mji wa Serikali iliyofanyika katika eneo la Mtumba, Dodoma. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.Pichani:Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) (wa nne kutoka kulia) akifurahia jambo wakati wa uzinduzi huo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Prof. Palamagamba John Kabudi, akibadilishana mawazo na baadhi ya mawaziri walioshiriki katika uzinduzi wa Mji wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli, akikata utepe katika jengo la Ofisi ya Rais, Utumishi, kuashiria uzinduzi wa jengo hilo.
Kanali Mbuge akipiga saluti kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kumpandisha cheo kuwa Brigadia Jenerali baada ya kushiriki kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya serikali
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Prof. Palamagamba John Kabudi, akiteta jambo na Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Dkt. Augustine Mahiga, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Prof. Palamagamba John Kabudi,akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Mtera, Mheshimiwa Livingstone Lusinde, kulia kwa waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afri
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Daniel Ndumbaro, akibadilishana mawazo na Mwanasheria wa Serikali Bungeni, Prof. Adelaus Kilangi.