Wizara ya Mambo ya Nje yakabidhi Madawati
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akikabidhi hundi ya michango ya madawati kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika tarehe 28 Julai, 2016 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chamazi iliyopo Mbagala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.