WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAPAN AWAANDALIA HAFLA MAALUM MAWAZIRI WANAOSHIRIKI MKUTANO WA SABA WA TIC

Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. Kono Taro akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi alipowasili kwenye Hoteli ya Royal Palace iliyopo jijini Yokohama kwa ajili ya kushiriki hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Mhe. Taro kwa heshima ya Mawaziri wanaoshiriki Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD 7) unaofanyika nchini humo kuanzia tarehe 28 hadi 30 Agosti 2019.

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAPAN AWAANDALIA HAFLA MAALUM MAWAZIRI WANAOSHIRIKI MKUTANO WA SABA WA TICAD

  • Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi, waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akisalimiana na Mawaziri wenzake akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Mhe. Dkt. Naledi Pandor (kulia) mara baada ya kumalizika kwa hafla maalum iliyoandaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. Taro.