Waziri Mkuu akutana na Watendaji wa Kampuni kubwa za China
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Kampini ya NORINCO ya nchini China, Bw. Zhang Gaunjie alipokutana naye kwa mazungumzo kuhusu uwekezaji nchini Tanzania.Mhe. Waziri Mkuu yupo nchi China kwa ajili ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC) unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 na 4 Septemba, 2018 jijini Beijing
Mhe. Waziri Mkuu akimkabidhi Bw. Gaunjie kitabu chenye taarifa kuhusu uwekezaji nchini Tanzania
Mhe. Waziri Mkuu akizungumza na Mwenyekiti wa Kampuni ya Syngning Guangzhou ya nchini China, Bw. WU Haineng. Kampuni ambao wana nia ya kufanyabiashara na Tanzania katika zao la mhogo
Mhe. Waziri Mkuu akiwa kwenye mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya GNSG ambao wana nia ya kuwekeza katika maeneo ya viwanda (Industrial Parks)
Mazungumzo yakiendelea