Waziri Mahiga apokea Nakala za Hati za Utambulisho
Waziri Mahiga apokea nakala za hati za utambulisho wa Balozi Mteule wa Oman na Iran.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Oman nchini Mhe.Ali A. Al Mahruqi alipowasili Wizarani kuwasilisha nakala za hati za utambulisho na kufanya makabidhiano kama inavyoonekana katika picha inayofuata
Pia Waziri Mahiga apokea nakala nyingine za hati za utambulisho wa Balozi Mteule wa Iran
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Iran Nchini Tanzania Mhe.Mousa Ahmed Farhang aliwasili Wizarani kuwasilisha nakala za hati za utambulisho.
Waziri Mahiga afanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania juu ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo hapa nchini
Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akizungumza mara baada ya kupokea nakala za hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Iran nchini Tanzania Mhe.Farhang.