Waziri Mahiga Aongoza Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC nchini Lesotho
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, amezihimiza taasisi za Serikali na za dini nchini Lesotho kudumisha amani na usalama kwenye kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi mkuu nchini hapa ili kuwezesha Serikali itakayoingia madarakani kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kwa ajili ya wananchi wa Lesotho.
Uchaguzi huo mkuu wa wabunge ambao ni wa tatu kufanyika ndani ya kipindi cha miaka mitano, unatarajiwa kufanyika tarehe 3 Juni 2017 ambapo vyama 26 kati ya 30 vilivyojiandikisha, vitashiriki kwenye kinyang’anyiro hicho cha kuchagua wawakilishi Bungeni.
Kwa mujibu wa Katiba ya Falme ya Lesotho, kiongozi wa chama kitakachoshinda viti vingi zaidi vya ubunge kwenye uchaguzi huo ndiye atakayeapishwa kuwa Waziri Mkuu na Kiongozi wa Serikali, ambapo mkuu wa nchi na mtawala mkuu anaendelea kuwa Mfalme Letsie III.
Dr. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mkuu wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC akizungumza na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho, Mhe. Jaji Mstaafu Lesao Lehohla (wa pili kutoka kulia) ali
Dkt. Mahiga na ujumbe wake wakikamilisha majumuisho ya mikutano mbalimbali waliyoifanyana na wadau .
Dkt Mahiga akiagana na wenyeji wake nje ya Tume Huru ya Uchaguzi.