Waziri Mahiga amuaga rasmi Balozi wa China nchini
Waziri Mahiga amuaga rasmi Balozi wa China nchini
Mhe. Waziri Mahiga akimkabidhi Balozi LU zawadi Maalum ya Nembo ya Taifa inayowakilisha utendaji uliotukuka wa Balozi LU
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akiwakaribisha Waziri Mahiga na Balozi LU kuzungumza kwenye hafla fupi ya kumuaga Balozi LU iliyofanyika Wizarani
Waziri Mahiga akizungumza na Balozi LU wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika Wizarani. Katika mazungumzo yao Mhe. Mahiga alimpongeza Balozi LU kwa utendaji wake wa kazi katika kipindi chote alichokuwa hapa nchini. Mhe. Mahiga alimwelezea Balozi LU kama mtu wa tofauti katika utendaji kazi na utekelezaji wake wa majukumu kwa kuwa alijitolea kikamilifu kuhakikisha ushirikiano kati ya Tanzania na China unaimarika na kukua zaidi
Picha ya pamoja kuhitimisha hafla ya kumuaga Balozi LU